1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boko Haram watwaa udhibiti jimbo la Niger

Iddi Ssessanga
4 Oktoba 2021

Kundi la kigaidi la Boko Haram limechukuwa udhibiti wa jamii kadhaa katika jimbo la Niger lililo kaskazini kati mwa Nigeria kwa kuwapatia fedha wanavijiji na kuwajumlisha katika safu zake ili kupambana na serikali.

https://p.dw.com/p/41EHf
Nigeria Region Borno Boko Haram
Picha: Audu Ali Marte/AFP/Getty Images

Suleiman Chukuba, mwenyekiti wa eneo la serikali la Shiroro katika jimbo la Niger, ambalo linapakana na Abuja, alisema wapiganaji wa Boko Haram walikuwepo katika wadi zisizopungua nane kati ya jumla ya 25.

Kundi hilo la itikadi kali lina ngome zake katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria na uwepo wake jimboni Niger, ambalo linapakana na eneo la mji mkuu wa shirikisho, unaashiria kuwa usaambaji wake unazidi kutia wasiwasi.

Hayo yanajiri wakati ambapo jeshi likisema kuwa juhudi zake za kupambana na uasi zinafanya kazi.