1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BONN: Waajiriwa wa Deutsche Telekom wagoma kufanya kazi

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1u

Mgomo wa wafanyakazi wa shirika la simu la Ujerumani “Deutsche Telekom” unaendelea,baada ya kama wafanyakzi 15,000 katika mikoa kadhaa kuondoka mahala pa kufanyia kazi zao.Huu ni mgomo mkuu wa kwanza kupata kufanywa katika historia ya shirika hilo la simu.Mgomo huo umeitishwa na chama cha wafanyakazi cha Ver.di baada ya baadhi kubwa ya wanachama wake kupiga kura ya kugoma kazi.Wafanyakazi hao wanaupinga mpango wa “Deutsche Telekom” wa kutaka kuhamisha nafasi za ajira zipatazo 50,000 katika sekta mpya za kuhudumia wateja ambako waajiriwa watapaswa kufanya kazi muda mrefu zaidi lakini kwa mishahara itakayokuwa midogo zaidi.