1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Dortmund bado ngangari katika Bundesliga

Sekione Kitojo
25 Februari 2019

Borussia  Dortmund yarejea katika  njia  ya  ushindi  katika  mbio za kuwania ubingwa  wa  ligi  ya  Ujerumani  kati  yake  na  Bayern Munich,

https://p.dw.com/p/3E4PH
Fußball Bundesliga Borussia Dortmund v Bayer Leverkusen Torjubel 3:1
Kikosi cha BVBPicha: Imago/DeFodi

Katika ligi  ya  Ujerumani  Bundesliga , viongozi  wa  ligi  hiyo  kwa sasa  Borussia  Dortmund  wameendelea kung'ang'ania  katika  mbio zao  za  kuwania  kutwaa  taji  la  ligi  ya  Bundesliga  msimu  huu kwa  ushindi  wa  mabao 3-2  jana  Jumapili  dhidi  ya  Bayer Leverkusen. 

Fußball Bundesliga Borussia Dortmund v Bayer Leverkusen
Mpambano mkali kati ya mlinzi wa BVB Manuel Akanji akipambana na Leon Bailey wa LeverkusenPicha: Imago/Kirchner

Ushindi  huu  wa  Borussia  Dortmund  ni  wa  kwanza katika  michezo  minne  ya  ligi  na  kuiweka  timu  hiyo  pointi  tatu juu  ya  msimamo  wa  ligi  ikiwatangulia  mabingwa  watetezi  Bayern Munich, ambayo  ilisogea  hadi  kuwa  sawa kwa  pointi  na  BVB baada  ya  ushindi  wao  wa  bao 1-0  dhidi  ya  Hertha Berlin  siku ya  Jumamosi.

Hivyo  ndivyo  mambo  yalivyokuwa  kati ya  Bayern  Munich  na Hertha  BSC  Berlin siku  ya  Jumamosi , lakini  Jacob Safari alifunga  safari  hadi  katika  uwanja  wa  Signal Iduna  Park mjini Dortmund  na  alishuhudia  pambano  kati  ya  Borussia  Dortmund ikipambana  na  Bayer 04  Leverkusen katika  mchezo uliokuwa  na mbinyo mkali  kwa  Dortmund wakati  wakijua  wazi  kwamba kufungwa  nyumbani  kutavunja  rekodi  yao  ya  kutofungwa nyumbani  katika  mchezo wa  ligi  msimu  huu, na  pia watakuwa wamefikiwa  kwa  pointi na  Bayern  Munich.

Fußball Bundesliga - Bayern München v Hertha BSC Torjubel
Wachezaji wa Bayern Munich wakimpongeza Javi Martinez kwa kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Hertha BerlinPicha: Reuters/A. Gebert

RB Leipzig kucheza Jumatatu

Leverkusen ilikuwa imepata  ushindi  katika  michezo  yake  minne  iliyopita chini  ya kocha  wao  mpya  Peter Bosz, ambaye  alitengana  na  BVB Desemba  mwaka  2017, wakati  kikosi  chake kilikuwa  katika kipindi chake  cha  muda  mrefu  bila  ushindi.

RB  Leipzig  iliyoko  katika  nafasi  ya  4 katika  msimamo  wa  ligi inajimwaga  dimbani  leo  Jumatatu  kupambana  na  Hoffenheim ikiwa  nyumbani. Lakini  timu ambayo inashangaza  kila  mchambuzi wa  kandanda  kwa  hivi  sasa  ni  VFL Wolfsburg  ambayo imeendelea  kupata  ushindi  tena  wa  kishindo  wiki  baada  ya wiki.

Fußball Bundesliga - Borussia Mönchengladbach v VfL Wolfsburg
Mpira ukielekea wavuni katika lango la Borussia Moenchengladbach katika mchezo wake na VFL WolfsburgPicha: Reuters/W. Rattay

Na wiki  hii  ilipata  ushindi  dhidi  ya  timu  iliyoko  katika  nafsi ya  tatu  Borussia  Moenchengladbach  wa  mabao 3-0 ikiwa  ugenini na  kuchupa  hadi  nafasi  ya  5  ikiwa  na  pointi 38.

Hata  hivyo timu  iliyofanya  vibaya wiki  hii  ni  Schalke 04  ambayo ilikubali  kipigo  cha  mabao 3-0 mikononi  mwa  Mainz 05 na  kubakia katika  nafasi  ya  13 na  kuchungulia  shimo  la  kushuka  daraja. Kutokana  na  hali  hiyo mkurugenzi  wa  spoti  wa  klabu  hiyo Christian Heidel ameamua  kuachia  ngazi msimu  huu  ukimalizika.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / rtre / ape /

Mhariri: Mohammed Khelef