1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yapata ushindi kwa tabu

Halima Nyanza30 Juni 2011

michuano ya kombe la Dunia la Soka la Wanawake inaendelea tena leo hapa Ujerumani kwa timu nne kujitupa uwanjani.

https://p.dw.com/p/11m8d
Mchezaji mahiri wa Brazil, MartaPicha: dapd

Katika mchezo wa jana Brazil iliweza kupata goli moja kwa bila dhidi ya Australia, ambayo pia ilionesha mchezo mzuri.

Katika mchezo wa awali hapo jana, wawakilishi wa Afrika, Guinea ya Ikweta ilifungwa bao moja kwa bila na Norway.

Fußball Frauen WM 2011 Norwegen Äquatorial-Guinea Gruppe D
Vuta nikuvutePicha: AP

Na kwa matokeo hayo ya jana, Brazil inaongoza katika kundi D, ikifuatiwa na Norway, Australia na Guinea ya Ikweta zikishika mkia, baada ya zote kufungwa.

Na katika mpambano wa leo wawakilishi wengine wa Afrika, Nigeria watapambana na wenyeji na mabingwa watetezi Ujerumani mjini Frankfurt.

Canada nayo itakutana na Ufaransa katika mji wa Bochum.

Mwandishi: Halima Nyanza(dpa, Reuters, afp)