1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brigid Kosgei avunja rekodi ya wanawake ya Marathon

Bruce Amani
14 Oktoba 2019

Mkenya Brigid Kosgei alivunja rekodi iliyodumu kwa miaka 16 ya mbio za marathon kwa wanawake. Kosgei alishinda mbio za Chicago Marathon jana Jumapili kwa kutumia muda was aa mbili, dakika 14 na sekunde 4.

https://p.dw.com/p/3RG60
USA Leichtathletik | Kosgei stellt Weltrekord bei Chicago-Marathon auf
Picha: Reuters/M. Segar

Baada ya kuivunja rekodi iliyowekwa na Muingereza Paula Radcliffe, Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema anaamini idadi yoyote ya washindani wanaweza kumpiku.

Kama mwanamke anaweza kujiandaa vyema, na asiwe na majeraha, anaweza kukimbia hata katika muda wa saa mbili na dakika 14, kupunguza hata kwa dakika mbili. Na kupunguza hadi hata saa mbili na dakika 12. Au kupunguza mpaka saa mbili dakika 13. Inawezekana kwa mwanamke kupunguza hiyo dakika. 

Ijapokuwa hakugusia uwezekano wa kuweka rekodi ya kukimbia marathon kwa muda wa 2.10.00, Kosgei ameweka wazi kuwa lengo laje ni kuhakikisha kuwa anaendelea kukimbia kwa kasi hata Zaidi.

Mimi nilikuja hapa kukimbia mbio zangu mwenyewe. Simtegemei mwingine. Ninazingatia tu mkondo wa kwenda na sio kumuangalia mwingine. Nililenga tu kukimbia kwa muda wangu. Nilitaka kuimarisha muda wangu wa binafsi na ndio maana nikakimbia leo.

Mkenya Lawrence Cherono alitimka na kumpiku Muethiopia Dejene Debela na kushinda mbio hizo kwa upande wa wanaume. Alitumia muda wa saa mbili, dakika tano, sekunde 45.