1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Vyombo vya habari

Bruce Amani

25 Julai 2017

Mfahamu Bruce Amani, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW

https://p.dw.com/p/2h6ON
DW Kiswahili Redaktuer Bruce Alakonya Amani
Picha: DW/L. Richardson
  1. Nchi ninayotokea: Kenya
  2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2011
  3. Nilivyojiunga na DW: Kwanza nilipata fursa ya mafunzo ya miezi sita na kisha baadaye nafasi ya kazi ikapatikana na nikaipokea.
  4. Kwa nini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Ni kitu nilitamani kukifanya tangu utotoni. Nilipenda sana kusikiliza redio na kuwafuatilia watangazaji mbalimbali pamoja na kazi zao
  5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Kama tu kazi nyingine yoyote, lazima uipende. Kisha uwe mbunifu na mkakamavu ili kutofautisha kazi yako na ya wengine. Kuwa mwandishi wa habari ni kitu ambacho unajifunza kila siku unapofanya kazi yenyewe. Hakuna anayefahamu kila kitu duniani!
  6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: mara nyingine unajikuta katikati ya hali ya machafuko au mikasa na majanga na hivyo kuyaweka maisha yako hatarini ili kupata habari. Lakini pia wakati mwingine, ukiwa katika mazingira hayo ya machafuko, mikasa na majanga, na pohitajika kufanya uamuzi wa kama kwanza utakuwa mwandishi wa habari kisha msamaria mwema au kwanza msamaria mwema kisha mwandishi wa habari!
  7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Nilifanya kazi wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2007 nchini Kenya, na hakika ulikuwa wakati mgumu sana kwangu kuwa mwanahabari!
  8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Mchezaji nguli wa kandanda kutoka Brazil, PELE