1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Mabadiliko ya hewa kuathiri zaidi nchi maskini

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBu

Repoti kuu ya Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa imetowa picha ya kutisha na kusema kwamba kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani kutaathiri sana mataifa ya kimaskini.

Baada ya mjadala wa muda mrefu Jopo la Kiserikali juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa linalokutana mjini Brussels Ubelgiji limekubaliana juu ya maudhui ya repoti hiyo ambayo inalaumu kwa kiasi kikubwa utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira unaofanywa na binaadamu.Inasema kuenea kwa jangwa,ukame na kupanda kwa viwango vya bahari kutaahiri mno maeneo ya nchi za joto kuanzia kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika hadi katika visiwa vya Pasifiki.

Waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel amezielezea juhudi za Marekani na China za kutaka kufuta baadhi ya vipengele vya waraka huo kuwa ni kashfa.Amezishutumu nchi hizo kwa uharibifu wa kisayansi na kuongeza kusema kwamba watu wana haki ya kujuwa taathira halisi za matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa.