1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Mazungumzo kati ya UU na Serbia kuanza karibuni.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvo

Kamishna anayehusika na upanuzi wa umoja wa Ulaya amesema kuwa mazungumzo ya kiushirika yanaweza kuanza na Serbia katika muda wa mwezi mmoja.

Olli Rehn ametoa matamshi hayo kufuatia mkutano kati ya rais wa Serbia aliyeko ziarani nchini Ujerumani Boris Tadic na kansela Angela Merkel . Akizungumza kwa niaba ya umoja wa Ulaya , Merkel amesema amefurahishwa na kukamatwa kwa jenerali wa zamani wa Bosnia, Mserbia ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya kuwahukumu wahalifu wa vita mjini The Hague.

Ujerumani kwa sasa inashikilia kiti cha urais wa umoja wa Ulaya.

Mkutano huo unakuja siku moja baada ya Zdravko Tolimir kukamatwa mashariki ya Bosnia.

Anatakiwa kwa kuhusika na mauaji ya mwaka 1995 ya kiasi cha Waislamu 8,000 wanaume na watoto mashariki ya mji wa Bosnia wa Srebrenica.

Tadic pia amerudia msimamo wa serikali yake wa kukataa mpango wa umoja wa mataifa ambao unatoa uhuru utakaosimamiwa kimataifa kwa jimbo la Serbia la Kosovo.