1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Ni mapema kuondosha vikwazo vya Umoja wa Ulaya

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCId

Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya,Javier Solana amekaribisha kuundwa kwa serikali mpya ya Wapalestina ya umoja wa kitaifa,lakini amesema,ni mapema mno kuamua ikiwa misaada ianze kutolewa tena.Umoja wa Ulaya umesema,upo tayari kuondosha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya serikali iliyokuwa ikiongozwa na Hamas,ikiwa serikali ya Wapalestina itakubali kuitambua Israel,itatangaza kuacha matumizi ya nguvu na itaheshimu makubaliano ya amani yaliyotiwa saini hapo awali.Kwa upande mwingine,Israel imekosoa mradi wa serikali mpya ya Wapalestina ambao haukuingiza suala la kulitambua taifa la Kiyahudi.Waziri mkuu mteule, Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas hapo awali, aliiwasilisha serikali hiyo mpya mbele ya Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah.