1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Serikali ya mpito ya Somalia yatakiwa ifanye mazungumzo na wanamgambo wa mahakama za kiislamu

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdS

Umoja wa Ulaya umeitaka serikali ya mpito ya Somalia ifanye mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu na wanamgambo wa mahakama za kiislamu.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amesema kutoroka kwa wanamgambo wa muungano wa mahakama za kiislamu kunatoa mwanya wa juhudi za kidiplomasia.

Waziri Steinmeier aliyasema hayo jana mjini Brussels Ubelgiji kufuatia mkutano wa wanachama wa Umoja wa Ulaya katika muungano wa kimataifa unaoshughulikia maswala ya Somalia.

Kundi la mataifa hayo, yakiwemo Marekani na Tanzania, litakutana kesho mjini Nairobi Kenya kujadili uwezekano wa kutuma kikosi cha kulinda amani nchini Somalia.