1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Ulaya yataka uchunguzi zaidi huko Darfur

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGc

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yametaka kuwepo kwa uchunguzi wa kimataifa juu ya ukiukwaji wa haki za binaadam huko Darfur.

Hii ni baada ya taarifa ya tume ya umoja wa mataifa kusema kuwa Serikali ya Sudan imeendelea na uhalifu wa kivita katika eneo hilo.

Mataifa hayo ya Ulaya imetaka kuundwa kwa tume ya watalaam itakayoichagiza serikali ya Sudan kuheshimu, maazimio yanayoitaka serikali hiyo kuheshimu haki za raia wa eneo la Darfur.

Inaarifiwa kuwa kiasi cha watu laki mbili wameuawa na wengine zaidi ya millioni mbili kuyahama makazi yao toka kuibuka kwa mzozo huko Darfur miaka minne iliyopita..

Serikali ya Sudan inashutumiwa kwa kuwaunga mkono wanamgambo wa Janjawidy, ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa ukatili wao.