1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya wafanya mawasiliano na serikali ya Palestina.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGv

Umoja wa Ulaya umekutana kwa mara ya kwanza na mjumbe wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Palestina.

Mjumbe wa umoja wa Ulaya katika mashariki ya kati, Marc Otte, amekuwa na mazungumzo mjini Gaza na waziri wa mambo ya kigeni wa Palestina Ziad Abu Amr jana Jumanne, ambaye ni mjumbe asiyekuwa na chama katika baraza la mawaziri.

Hata hivyo , umoja wa Ulaya umekataa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya serikali ya Palestina hadi pale itakapoitambua Israel, kukana matumizi ya nguvu na kuheshimu makubaliano yaliyokwisha fikiwa.

Marekani, Russia na Umoja wa mataifa pamoja na Ufaransa, Austria na Ubelgiji zimetangaza pia hatua kuelekea kuanzisha tena mahusiano na wajumbe ambao si wa chama cha Hamas wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Palestina.