1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUDAPEST: Watu wakamatwa katika maandamano ya upinzani mjini Budapest nchini Hungary

24 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzc

Waandamanaji kiasi ya 100 wamekamatwa na polisi na wengine 128 wamejeruhiwa katika ghasia zilizotokea kati ya waandamanaji na polisi wa usalama wakati zikifanyika sherehe za mwaka wa 50 tokea mapinduzi ya utawala wa kikoministi. Viongozi wamesema polisi wameingilia kati kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia gesi za kutoa machozi na risase za mpira.

Polisi 19 wamejeruhiwa pia katika ghasia hizo.

Uasi nchini Hungary ulianza tarehe 23 Oktoba mwaka 1956. Ulizimwa na vifaru vya kijeshi vya Sovieti ya zamani tarehe 4 Novemba na hivyo kuhakikisha nchi hiyo kuendelea kuwa kibaraka cha Sovieti ya zamani hadi uliposambaratika ukoministi mwaka wa 1989.