1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura. Mwasisi wa CNDD kuondolewa kinga.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6b

Bunge la Burundi limemvua kinga ya ubunge mwanasiasa maarufu nchini humo Hussein Rajab. Hii imetokea baada ya bunge la nchi hiyo kukubali ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kutaka Rajabu aondolewe kinga hiyo.

Kwa muda wa siku mbili Rajab amekuwa akifika mbele ya mahakama baada ya kutuhumiwa na polisdi ya nchi hiyo kwamba alikuwa na nia ya kupanga uasi.

Hussein Rajab ni mmoja kati ya wanasiasa waasisi wa chama kilichokuwa cha waasi zamani cha CNDD FDD ambacho hivi sasa kiko madarakani.