1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga yashuhudia mvua ya mabao

30 Oktoba 2023

Jumla ya mabao 42 yalipachikwa wavuni katika mechi za mzunguko wa 9, idadi ya juu zaidi kuandikishwa tangu msimu ulipoanza.

https://p.dw.com/p/4YCjs
Fußball Bundesliga FC Bayern München v Darmstadt 98 | Tor Kane vom Mittelkreis
Harry Kane akipiga shuti katika mechi ya Bundesliga dhidi ya DarmstadtPicha: Tom Weller/dpa/picture alliance

Siku ya Jumamosi Bayern Munich waliicharaza Darmstadt mabao 8 bila jibu katika uga wa nyumbani Allianz Arena. Jumla ya kadi tatu nyekundu zilionyeshwa wachezaji Joshua Kimmich wa Bayern, Klaus Gjasula na Matej Maglica wa Darmstadt.

Soma pia: Kane atetemesha Bundesliga

Mshambuliaji Harry Kane aliendeleza rekodi nzuri ya ufungaji mabao na kwa mara ya pili katika Bundesliga akafunga mabao matatu kwenye mechi moja.

"Umekuwa mwanzo mzuri kufikia sasa, nadhani tumekuwa na mchezo mzuri leo, sio mimi tu lakini timu yote. Ninafuraha na ninafurahia kila dakika ya uwepo wangu hapa na klabu pamoja na mashabiki. Na kufunga Hatrick katika uga wa nyumbani ni hisia ya kipekee." Alisema Kane baada ya mechi.

RB Leipzig ilisherehekea ushindi mnono wa 6-0 nyumbani dhidi ya FC Köln, Dortmund walitoka nyuma mara mbili na kuambulia pointi moja katika mechi kali iliyokamilika kwa sare ya 3-3 dhidi ya Eintracht Frankfurt katika uwanja wa Deutsche Bank Park.

Leverkusen moto wa kuotea mbali

Florian Wirtz alifunga bao maridadi na kufungua njia kwa vijana wa Xabi Alonso wa Bayer Leverkusen kuwalaza Freiburg 2-1 jana Jumapili na kurudi kileleni mwa jedwali la Bundesliga. 

Fußball Bundesliga Bayer Leverkusen - SC Freiburg | Jubel Florian Wirtz
Leverkusen wakisherehekea ushindi dhidi ya Freiburg. Bundesliga mechi ya mzunguko wa 9.Picha: Horst Mauelshagen/pepphoto/IMAGO

Hoffenheim iliendeleza matokeo mazuri ugenini kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji wao Stuttgart. Borussia Moenchengladbach ilivuna mabao 2-1 dhidi ya Heidenheim. Union Berlinikaendelea kutandikwa kwa kipigo cha 2-0 kutoka kwa Werder Bremen. Bochum na Mainz zikatoka sare ya 2-2 na Ausburg ikaifunga Wolfsburg 3-2.