1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge kuu la Ujerumani lakubali wanajeshi wa Ujerumani wasalie mwaka mmoja zaidi Afghanistan

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GM

Berlin:

Bunge la shirikisho la jamhuri ya Ujerumani,Bundestag,limeunga mkono kwa wingi mkubwa ,shughuli za wanajeshi wa Ujerumani Bundeswehr zirefushwe kwa mwaka mmoja nchini Afghanistan.Wanajeshi 3500 wa Ujerumani wanakutikana zaidi katika eneo la kaskazini la Afghanistan.Wanajeshi hao ni sehemu ya wanajeshi wa kimataifa –ISAF-wanaoongozwa na jumuia ya kujihami ya magharibi NATO ambao jukumu lao ni pamoja na ujenzi mpya wa Afghanistan.wabunge 454 wameunga mkono mswaada huo pakiwepo pia kura za upande wa upinzanai wa FDP.Wabunge 79 wamepinga na 48 hawakupiga kura upande wowote-wengi wao ni wabunge wa chama cha walinzi wa mazingira Die Grüne.Waziri wa ulinzi Franz Josepf Jung anasema:

„Nimeridhika na matokeo ya kura bungeni.Tumepata wingi mkubwa,asili mia 78 ya wabunge wanatuunga mkono.Huu ni ushahidi wa imani yao kwa shughuli za wanajeshi wa Bundeswehr,wake kwa waume.Uungaji mkono huu ni muhimu kwa shughuli zao za kuimarisha hali ya utulivu na amani nchini Afghanistan na kwa namna hiyo,ni mchango pia kwa usalama wetu.“

Upande wa upinzani wa mrengo wa shoto, Die Linke unahoji, shughuli za Bundeswehr hazikusaidia kuwavunja nguvu wataliban.