1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge la Marekani kupigia kura miswada ya msaada

Tatu Karema
20 Aprili 2024

Bunge la Marekani linatarajiwa leo kuipigia kura miswada minne ya msaada kwa Ukraine, Israel na Taiwan pamoja na uwezekano wa kupigwa marufuku kwa mtandao wa kijamii wa Tik Tok

https://p.dw.com/p/4f0Lb
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba kuhusu msaada wa dola bilioni 95 kwa mataifa ya nje mnamo Februari 13,2024 mjini Washington
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Kura ya miswada hiyo ya takribani dola bilioni 95 za msaada kwa mataifa ya kigeni pamoja na ununuzi wa silaha inatarajiwa kupigwa baadaye leo, huku Spika Mike Johnson wa chama cha Republican akihitaji uungwaji mkono wa chama cha Democrat kuipitisha.

Soma pia: Marekani yaihakikishia Ukraine kupata msaada wa kijeshi

Miswada hiyo inatokana na mchakato wa miezi kadhaa ya majadiliano na shinikizo kutoka kwa washirika wa Marekani pamoja na maombi ya mara kwa mara ya msaada kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Marekani haijaidhinisha msaada mkubwa kwa Ukraine kutokana na mvutano wa kisiasa 

Marekani imekuwa mfadhili mkubwa wa kijeshi kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi, lakini bunge la nchi hiyo halijaidhinisha msaada wa kiwango cha juu kwa taifa hilo kwa takribani mwaka mmoja na nusu kutokana na mvutano wa kisiasa.