1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush akutana na viongozi wa Wapalestina

10 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CnfL

RAMALLAH

Rais George W. Bush wa Marekani leo amekutana na viongozi wa Wapalestina katika mji wa Ramallah akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu katika eneo hilo kwa lengo la kuupa nguvu mchakato wa amani kati ya Israel na Wapalestina uliofufuliwa upya.

Rais Bush amefanya mazungumzo na Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina pamoja na kukutana na Waziri Mkuu Salam Fayad na msuluhishi mkuu wa Palestina Ahmed Qorei na baadae alikuwa na mkutano na waandishi wa habari.

Bush aliwasili Israel hapo jana na kuwa na mazungunzo na Waziri Mkuu Ehud Olmert.

Rais Bush leo mchana atautembelea mji wa Bethlehem katika Ukingo wa Magharibi na hapo kesho anatazamiwa kuelekea Kuwait kituo chake cha pili cha ziara yake ya siku nane Mashariki ya Kati.