1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUSH-LIBERIA

Kalyango, Siraj22 Februari 2008

Asema ataipiga jeki sekta ya elimu ya Liberia

https://p.dw.com/p/DBL3
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, kushoto, akizungumza na rais wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf.Picha: AP


Rais George W Bush wa Marekani amaeanza ziara yake rasmi nchini Liberia ,ambacho ni kituo chake cha tano na cha mwisho katika ziara yake barani Afrika.


Liberia ina umuhimu wa kihistoria na kimkakati kumfanya rais Bush aitembele.

Awali ya yote Bush,amevunja daftari ya kihistoria kwa rais wa Marekani kuhusiana na nchi hiyo . Hii ndio ziara ya rais wa Marekani ya kwanza kwa kipindi cha miaka 30.



Liberia ndio jamhuri ya kwanza kuundwa barani Afrika.Iliundwa miaka ya 1820 .Walioliunda walikuwa watumwa waliochiliwa huru kutoka Marekani.


Pia nchi hiyo kwa sasa ndio taifa pekee la kiafrika linaloongozwa na mwanamake aliechaguliwa rasmi.


Bendera za nchi hizo mbili zinafanana jambo tofauti ni kuwa ya Liberia ina nyota moja katikati ilihali ya Marekani ina nyota 50.


Umuhimu wa Liberia pia ni kuwa mbali na kuwa ndio kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika ambapo ametembelea mataifa matano,lakini pia ndio taifa pekee barani Afrika ambalo limekubali kujengwa kituo ama kambi ya kijeshi ya Marekani.

Jambo hilo aliligusia kijuujuu kabla ya kuondoka Ghana,alipoondoa uvumi wa kuwa anataka Ghana nayo itoe ruhsa wa kituo cha kijeshi kuhusu Afrika cha Africom.


Kituo hicho,licha ya Bush kutokiri hadharani lakini habari za kuaminika zinasema kinatarajiwa kuwekwa nchini Liberia ambako yuko huko kwa sasa.


Bush akiandamana na mkewe pamoja na waziri wake wa mashauri ya kigeni-Condoleeza Rice-hakwenda huko mikono mitupu,bali ameipiga jeki sekta ya elimu kwa kutoa vitabu vya kusomea millioni moja ,viti na meza vya wanafunzi laki moja.


Punde tu baada ya kuwasili Bush amemwambia rais Ellen Johnson Sirleaf kuwa,anataka kuwakarabati baada ya kukabiliwa na kipindi kigumu na badala yake anawataka waishi maisha ya amani na raha.


Afisa wa Ikulu ya Marekani amesema kuwa msaada huo utaanza kuwasili huko mwanzoni mwa mwaka ujao.

Liberia imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mda mrefu,vya mwishi vikiwa vilimalizika mwaka wa 2003.


Watu wanaofikia laki tatu,walipoteza maisha yao katika machafuko yaliendelea kwa kipindi cha miaka 14 na kumalizika mwaka wa 2003.Kabla ya machafuko hayo kumalizika Umoja wa Mataifa ulituma kikosi cha kulinda amani nchini humo cha wanajeshi wanaofikia elf 14,kwa lengo la kumaliza machafuko.

Baado Umoja wa Mataifa unawajibika na kushughulikia usalama wa nchi hiyo ambapo jeshi lake changa baado linapewa tu mafunzo.

Barabara zote zinazoingia mjini Monrovia zilifungwa kwa ajili ya usalama wa Bush.


Tangu rais Sirleaf achukue hatamu mwaka wa 2006,Marekani iliahidi kutoa dola millioni 300 kwa ajili ya ukarabati.

Na chini ya mpango wa Marekani wa kusaidia elimu barani Afrika-Liberia inapokea kitita cha dola millioni 600 hadi mwaka wa 2010.