1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAF yaingilia mzozo wa timu ya wanawake ya Afrika Kusini

Bruce Amani
5 Julai 2023

Mkuu wa shirikisho la kandanda Afrika - CAF Patrice Motsepe ameingilia kati kusuluhisha mzozo kati ya timu ya wanawake ya Afrika Kusini itakayoshiriki Kombe la Dunia la 2023 na chama cha kandanda nchini humo.

https://p.dw.com/p/4TQx2
Patrice Motsepe
Mkuu wa Shirikisho la soka Afrika CAF Patrice MotsepePicha: Weam Mostafa/Sports Inc/empics/picture alliance

Mkuu wa shirikisho la kandanda Afrika - CAF Patrice Motsepe ameingilia kati kusuluhisha mzozo kati ya timu ya wanawake ya Afrika Kusini itakayoshiriki Kombe la Dunia la 2023 na chama cha kandanda nchini humo. Chanzo cha CAF kimesema mzozo huo unaohusu Banyana Banyana ni fedheha kubwa sio tu kwa Afrika Kusini, bali Afrika nzima. Kimesema ilibidi hatua ichukuliwe haraka, huku baadhi ya wachezaji wakitarajiwa kuondoka leo kueleeka New Zealand. Australia na New Zealand wanaandaa kwa pamoja Kombe la Dunia na mabingwa wa AFRIKA, Afrika Kusini, Morocco, Nigeria na Zambia wanawakilisha bara hilo. Motsepe alisaidia kutatua masuala kuhusu mikataba, ambayo wachezaji walisema haikujumuisha dola 30,000 kama malipo ya kushiriki kwenye kinyang'anyiro hicho zilizoahidiwa na FIFA kwa kila mmoja wa kikosi hicho chenye wachezaji 23. Hii ilisababisha timu hiyo kususia mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya Botswana Jumapili iliyopita.