1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAMP DAVID: Karzai akamilisha ziara ya siku mbili Marekani

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbT

Marais George W. Bush wa Marekani na Hamid Karzai wa Afghanistan wameapa kuliangamiza kundi la Taliban ambalo rais Karzai amelitaja kuwa sio tishio kwa serikali yake.

Rais Karzai aliyasema hayo wakati alipokutana na rais Bush katika eneo la Camp David karibu na mji wa Washington nchini Marekani.

Viongozi hao pia wamekubaliana juu ya kutotolewa ridhaa ya aina yoyote kwa kundi la Taliban linalowashikilia mateka 21 raia wa Korea Kusini.