1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa kadhaa yajiunga na kesi ya mauaji ya Myanmar

John Juma
17 Novemba 2023

Mahakama ya kimataifa ya jinai imesema nchi za Canada, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Uingereza zimeungana katika kesi ya mauaji ya halaiki ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya walio wachache,

https://p.dw.com/p/4Z1ml
Uholanzi | Mahakama ya ICJ | 
Mahakama ya Kimataifa ya haki ICJPicha: International Court of Justice/UN Photo/Wiebe Kiestra

Mataifa hayo yamewasilisha tamko la pamoja la kuingilia kati kesi hiyo katika mahakama hiyo ya kimataifa ya Haki (ICJ). Nchi hizo zimetaja masilahi yao ya pamoja kutaka mkataba wa mwaka 1948 wa kuzuia mauaji ya halaiki na kuadhibiwa kwa uhalifu huo kuzingatiwa.

Kiongozi wa Myanmar asema uasi unatishia kulisambaratisha taifa

Tania von Uslar, afisa wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kupitia ukurasa wake wa X kwamba wanaangazia haswa ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulihitimisha kuwa kampeni ya jeshi la Myanmar ya mwaka 2017 iliyowafukuza Warohingya 730,000 waliokimbilia nchi jirani ya Bangladesh ilikuwa imejumuisha "vitendo vya mauaji ya kimbari".