1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS: Chavez wa Venezuela ajinyakulia ushindi wa rais

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmh

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa rais uliofanywa nchini Venezuela siku ya Jumapili huonyesha kuwa rais wa hivi sasa,Hugo Chavez mwenye siasa za mrengo wa shoto,anaongoza kwa uwingi mkubwa baada ya asilimia 78 ya kura kuhesabiwa.Mpinzani wake mkuu,gavana wa jimbo,Manuel Rosales amekubali kushindwa.Rosales,wakati wa kampeni zake za uchaguzi,alimshutumu Chavez kuwa anaiongoza nchi hiyo kuwa kama Kuba,ikitawalwa na mtu mmoja. Idadi kubwa ya watu walijitokeza kupiga kura hiyo jana.Kwa maoni ya upande wa upinzani,utaratibu wa kupiga kura umeridhisha.