1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Caracas. Kituo cha TV kufungwa.

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxZ

Polisi nchini Venezuela wamevunja maandamano ya upande wa upinzani baada ya mamia ya watu kuingia mitaani wakimshutumu rais Hugo Chavez kwa kufunga kituo kimoja cha Televisheni.

Polisi wa kutuliza ghasia walitumia mabomba ya maji na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wapinzani dhidi ya kufungwa kwa kituo hicho cha Televisheni cha RCTV, kituo ambacho televisheni yake inaangaliwa na watu wengi zaidi nchini humo.

Kituo hicho kinachomilikiwa na mtu binafsi kilikuwa kinatarajiwa kusitisha matangazo yake wakati wa usiku jana Jumapili katika hatua ambayo rais Chavez amesema ni kuingiza udemokrasi katika utangazaji. Wakosoaji wamesema kuwa rais huyo anajaribu kukandamiza mawazo ya watu wanaoipinga serikali.