1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS: Waandamanaji wamuunga mkono Rais Chavez

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvE

Maelfu ya watu wameandamana barabarani katika mji mkuu wa Venezuela,Caracas kumuunga mkono Rais Hugo Chavez.Maandamano hayo yamefanywa baada ya Chavez kuchukua hatua iliyozusha mabishano, ya kuifunga stesheni ya televisheni ya upande wa upinzani,ambayo katika mwaka 2002 waziwazi ilitoa mwito wa kumuondoa Chavez madarakani.Waziri wa mawasiliano ya simu,Jesse Chacon amesema,rais anafanya mageuzi ya kidemokrasia katika mfumo wa matangazo.Wapinzani wa kisiasa lakini wanasema, hatua iliyochukuliwa na Rais Chavez inakiuka uhuru wa vyombo vya habari.