1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Castro kuwania ubunge nchini Cuba

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVtE

HAVANA.Rais Fidel Castro ameteuliwa kuwania kiti cha ubunge nchini Cuba katika uchaguzi mkuu ujayo na kuashiria kuwa kiongozi huyo hajawa tayari kung´atuka katika siasa na kwamba huenda akarejea tena katika urais.

Castro ambaye hajaonekana hadharani toka alipokabidhi madaraka kwa mdogo wake Raul mwezi Julai mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji,ni miongoni mwa wagombeaji wa ubunge katika uchaguzi utakaofanyika January mwakani.