1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA yahofia kuchezewa rafu

29 Oktoba 2010

Zimebaki siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu wa Urais nchini Tanzania.

https://p.dw.com/p/PpkI
Kampeni za uchaguzi nchini TanzaniaPicha: DW

Ikiwa siku tatu zimebakia kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa urais, wa bunge na madiwani huko Tanzania, chama cha Chadema kimetaja malalamiko yake kwa tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo kuhusu daftari la wapiga kura lililotolewa na tume hiyo kwa njia ya kompyuta. Othman Miraji ameyapata hayo pale alipomhoji meneja mkuu wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho, Profesa Mwesige Baregu.

Mwandishi: Othman Miraji

Mpitiaji: Josephat Charo

Na huko Zanzibar, kinyume na chaguzi kuu tatu zilizopita za urais na Baraza la wawakilishi, mara hii, hadi hivi sasa, kampeni za uchaguzi zimefanyika kwa ushwari na ustaarabu.

Mwenzetu wa Deutsche Welle, Mohammed Abdulrahman, aliyoko Unguja mjini, anatupa sura ilivyo katika kisiwa hicho cha Karafuu...

Kinyume na chaguzi kuu tatu zilizopita za urais na Baraza la wawakilishi, mara hii, hadi hivi sasa, huko Zanzibar kampeni za uchaguzi zimefanyika kwa ushwari na ustaarabu.

Mwandishi: Mohamed Abdulrahman

Mpitiaji: Othman Miraji