1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Baiskeli - UCI chamchagua rais mpya

28 Septemba 2013

Kiongozi mpya wa Chama cha Uendeshaji Baiskeli Ulimwenguni – UCI Brian Cookson ana kibarua kigumu kuhakikisha kuwa hadhi ya mchezo huo ambayo imechafuliwa kwa muda mrefu inarekebishwa

https://p.dw.com/p/19pob
Picha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Cookson atataraji kuwa mwendesha basikeli aliyekabiliwa na kashfa kubwa ya matumizi ya dawa za kulevya Lance Armstrong anaweza kutekeleza jukumu kubwa katika mchakato wa “ukweli na maridhiano” na kusaidia kuponya vidonda vya mchezo huo.

Cookson alimpiku kiongozi anayeondoka Pat McQuaid katika wadhifa wa urais wa UCI baada ya mchakato wa uchaguzi uliokumbwa na hisia kali jana Ijumaa. Wakati Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 62 akitaraji ushirikiano kamili kutoka kwa McQuaid kama uchunguzi utaanzishwa kuhusiana na ufisadi ndani ya chama hicho, Armstrong huenda akawa mmoja wale ambao Cookson atatangulia kuwatolea mwito.

Kukiri Armstrongkwamba alitumia dawa za kusisimua misuli katika taaluma yake yote, baada ya kupigwa marufuku ya maisha katika mchezo huo mwaka mmoja uliopita, kuliharibu hata zaidi hadhi ya uendeshaji baisikeli.

Kampeni ya Cookson ilihusu wito wa kuanzishwa shirika la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni ambalo litakuwa huru bila uhusiano na UCI, kwa sehemu, kutokana na madai kwamba McQuaid na rais wa zamani wa UCI Hein Verbruggen walishirikiana katika siku za nyuma, kuficha habari kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Josephat Charo