1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUP yaridhia kurejea serikalini Ireland Kaskazini

30 Januari 2024

Chama kikubwa cha siasa cha Ireland Kaskazini cha Democratic Union, DUP,kimesitisha uamuzi wake wa kususia kuwa sehemu ya serikali, msimamo ulioacha Ireland Kaskazini bila utawala kwa muda wa miaka miwili.

https://p.dw.com/p/4bqif
Jeffrey Donaldson
Mkuu wa chama hicho kinachopinga hisia za kujitenga kwa Ireland na Uingereza Jeffrey Donaldson Picha: DW

Mkuu wa chama hicho kinachopinga hisia za kujitenga kwa Ireland na Uingereza Jeffrey Donaldson amesema kamati kuu ya DUP imeridhiamapendekezo ya kurejea serikalini baada ya mashauriano marefu yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

Amesema makubaliano yaliyofikiwa na serikali kuu mjini London yanatoa msingi wa kupatikana serikali ya Ireland Kaskazini ndani ya muda siku mbili zinazokuja. 

DUP ilisusia kuendelea kuwa ndani ya serikali ya Ireland Kaskazinimnamo 2022 kufuatia mvutano uliotokana na kanuni za biashara za baada ya mchakato wa Brexit.

Soma pia:Biden: Mustakabali wa Ireland Kaskazini ni mustakabali wa Marekani

Tangu wakati huo kimekataa kushirikiana na chama cha kizalendo cha Sinn Fein. Chini ya mkataba wa amani uliotiwa saini miaka 25 iliyopita, vyama hivyo viwili ni lazima viwakilishwe ndani ya serikali ya Ireland Kaskazini.