1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUreno

Raia wa Ureno wafanya uchaguzi wa mapema

Lilian Mtono
10 Machi 2024

Raia nchini Ureno wanapiga kura Jumapili hii katika uchaguzi wa mapema huku kura za maoni zikionyesha chama cha mrengo wa kulia cha Democratic Alliance kukitangulia kile cha Kisoshalisti.

https://p.dw.com/p/4dMA8
Ureno | Uchaguzi
Maria Gloria Ribeiro,mtawa anayeonekana akipiga kura katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi mkuu huko Lisbon, Ureno, Machi 10, 2024Picha: Violeta Santos Moura/REUTERS

Uchaguzi huo wa Ureno huenda ukaifanya nchi hiyo kujiunga na wimbi la mrengo wa kulia kote Ulaya baada ya miaka minane ya utawala wa Kisoshalisti. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi katika taifa hilo lenye karibu watu milioni 10.

Wachambuzi wanaonya kuwa matokeo ya uchaguzi huo, ambao ni wa pili katika miaka miwili, bado yako wazi ikizingatiwa idadi kubwa ya wapiga kura ambao hawajaamua.

Uchunguzi wa mwisho wa maoni uliochapishwa Ijumaa ulionesha chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia cha Democratic Alliance - AD kikiwa mbele ya chama cha Kisoshalisti cha PS, kwa tofauti ya kura chache lakini kikipungukiwa na wingi wa viti bungeni.

Hiyo inaweza kukifanya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Chega kuwa muhimu katika kuunda serikali ya muungano.