1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha SPD chajadiliana juu ya kuufufua umaarufu wake

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAOt

NUREMBURG

Chama cha Social Demokratic nchini Ujermani kinakutana mjini Nuremburg kusini mwa Ujerumani kujadili mipango yake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.Wajumbe wa chama hicho cha SPD watajadiliana njia za kuufufua umaarufu wa chama chao baada ya uchunguzi wa maoni kuonyesha kwamba chama hicho kimepungua umaarufu tangu kilipoingia madarakani katika serikali ya mseto na chama cha kansela Angela Merkel cha CDU kiasi cha miaka mitatu iliyopita. Uchunguzi huo wa maoni umeonyesha kwamba wapiga kura wamevunjwa moyo na mgawanyiko ulioko ndani ya chama hicho.