1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto za kisiasa zinazowakabili Wakristo wa Madhehebu ya Maronite nchini Lebanon.

Halima nyanza12 Desemba 2007

Waumini wa madhehebu ya Maronite nchini Lebanon, ambako kikatiba ndiko hutoka Rais, wanakabiliwa na changamoto ya mvutano ya ndani na pengo la nafasi ya juu ya uongozi, baada ya aliyekuwa akiishikilia kumaliza muda wake.

https://p.dw.com/p/Capv
Rais aliyemaliza muda wake nchini Lebanon, Emile Lahoud.Picha: AP

Nafasi hiyo ya uongozi wa juu imekuwa wazi tangu Rais wa Lebanon Emile Lahoud, kumaliza kipindi chake cha kuongoza nchi hiyo Novemba 23 mwaka huu, ambapo pia kumekuwa na mvutano wa kugombea madaraka kati ya wabunge wengi wanaoungwa mkono na magharibi pamoja na wapinzani wanaoungwa mkono na Syiria.

Bunge la nchi hiyo, tangu mwezi Septemba limeahirisha mara nane kikao cha kumchagua rais wa nchi hiyo, ingawa Desemba 17 imetajwa kuwa siku yakufanyika uchaguzi huo.

Lakini hata hivyo wanasiasa nchini humo wanaamini kuwa upigaji kura huo unaweza kuahirishwa tena hadi mwaka ujao.

Mwandishi wa Makala maalum Rosana Bou Mouncef anaelezea kuwa wakristo nchini humo kwa sasa wananafasi aliyioiita kuwa ni ya pekee kuchagua Rais aliye imara, kwa kuzingatia kuwa upigaji kura huo utakuwa ni wa kwanza tangu kumalizika kwa miongo mitatu ya utawala wa kijeshi wa Syria nchini Lebanon.

Mwandishi huyo amenukuliwa akisema kuwa kwa mara ya kwanza rais mpya hatateuliwa tena na Damascus na kwamba kiongozi huyo lazima akabiliane na changamoto na awakilishe Wakristo kikamilifu.

Lebanon taifa pekee la kiarabu lenye kiongozi mkuu wa nchi mkristo, halijawahi kufanya sensa ya kuhesabu watu tangu mwaka 1932 ambapo idadi ya raia wakristo nchini humo ilikuwa nia asilimia 54 ya watu wote nchini humo.

Hata hivyo baadaye wakristo walikadiriwa kuwa asilimia 36 ya wakaazi milioni nne, wakati mahehebu ya waislamu wa Sunni na Shia ni asilimia 29 kwa kila moja.

Uongozi ni jambo linalosumbua sana wakristo wa madhehebu ya Maronite ambao ndio wanakotoka jamii ya wakristo wengi wa Lebanon.

Kwa kufuata katiba ya nchi hiyo madhehemu ya Suni ndio yanayotoa Waziri mkuu na madhehebu ya Shia yamekuwa yakitoa Spika wa Bunge.

Wakristo wengi nchini Lebanon wamekuwa wakihisi kana kwamba wametupwa tangu mwaka 1989, wakati wa makubaliano ya Taef ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyoanza mwaka 1975 na kumalizika mwaka 1990 na kupunguza nguvu ya rais.

Nayla Tueni mtoto wa aliyekuwa mbunge nchini humo Gebran Tueni anasema kuwa Lebanon inahitaji Rais aliyeimara, ambaye anajivunia ukristo wake.

Anasema pia rais mpya ni lazima awasaidie wakristo nchini humo kuweza kujiamini.