1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changamoto za kiufundi bado zipo kuandaa uchaguzi DRC

Saleh mwanamilongo20 Desemba 2018

Tume huru ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza kwamba kuna changamoto za kiufundi ambazo huenda zikasababisha kuahirishwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja.

https://p.dw.com/p/3AQKc
Demokratische Republik Kongo Wahlmaschine
Picha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Tume huru ya uchaguzi imelezea kwamba kila kitu kimefanywa ili kuakikisha kwamba uchaguzi umefanyika Jumapili Desemba 23, lakini bado kuna changamoto za kiufundi kwa ajili ya jiji la Kinshasa ambazo huenda zikasababisha kuahirishwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja. Tayari mgombea wa upinzani Martin Fayulu amesema hawezi kukubali hatua yeyote ya kuahirishwa kwa uchaguzi.

Corneille Nangaa ambaye ni mwenyekiti wa tume huru ya uhaguzi,CENI, ameitisha mkutano na waandishi habari saa tisa alasiri Kinshasa ili kuelezea hatua iliofikiwa na CENI, katika maandalizi ya uchaguzi.

Lakini kwa mara ya kwanza kabisa, msemaji wa tume huru ya uchaguzi ameelezea kuhusu uwezekano wa kuahirishwa kwa siku chache uchaguzi huo. Akizungumza na idhaa ya kifaransa ya BBC, Jeanpierre Kalamba amesema kwamba kila kitu kimefanywa ili uchagui huo ufanyike Jumapili lakini changamoto za kiufundi kwa ajili ya mji wa kinshasa zinaweza kusababisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo kwa kipindi kifupi kabisa.

 "Tunatathmini taratibu hii kila dakika na kila saa,ili kujuwa ikiwa kil akitu kinakwenda sambamba na ikiwa haitowezekana tutarejea kwa wagombea wote na kuwafahamisha hilo. Ikiwa itahitajika siku 4,5 ,7 au siku 10 au 14 kuandaa vizuri uchaguzi huo kuna ubaya gani kufanya hivyo? Hatuwezi kuanguka katika mtego wa kuheshimu tarehe huku uchaguzi umefanyika vibaya". Amesema Corneille.

kuungua kwa ghala yake ya vifaa vya uchaguzi kwa ajili ya jiji la Kinshasa ndio sababu kubwa ya kuchelewa kwa taratibu hiyo
kuungua kwa ghala yake ya vifaa vya uchaguzi kwa ajili ya jiji la Kinshasa ndio sababu kubwa ya kuchelewa kwa taratibu hiyo.Picha: AFP/Getty Images/J. Wessels

Hata hivyo CENI bado inaendelea kuamini kwamba uchaguzi utafanyika Jumapili. Tume huru ya uchaguzi imeelezea kwamba kuungua kwa ghala yake ya vifaa vya uchaguzi kwa ajili ya jiji la Kinshasa ndio sababu kubwa ya kuchelewa kwa taratibu hiyo. Mbali na hilo kuna pia fomu za kuandika matokeo ambazo zilichelewa kuwasili hapa kutokea nchini Afrika ya kusini.

Mgombea Martin Fayulu alielezea kwamba yeye na vuguvugu linalomuunga mkono LAMUKA hawawezi kukubali hatua yeyote ya kuahirishwa kwa uchaguzi.

Kanisa katoliki limetangaza kwamba liko tayari kuwatawanya wasizamazi wake 40.000 kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Tume ya haki na amani ya kongamano la maaskofu wa Kongo, limesema mafunzo ya watizamaji wake kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika.

Serikali ya Kongo, haikuwaalika watizamaji wa Umoja wa Ulaya na wale wa kituo cha Carter. Lakini Umoja wa Afrika na Jumuiya ya SADC vimetuma watizamaji wake wa uchaguzi. Kampeni ya uchaguzi imetarajiwa kumalizika kesho Ijumaa.

Mwandishi: Saleh mwanamilongo,Dw Kinshasa.