1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chavez aonja kushindwa.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW4E

Caracas. Wapiga kura wa Venezuela wametupilia mbali mageuzi ya katiba ambayo yangempa rais Hugo Chavez haki ya kuweka uchumi wa kisoshalist katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta na kuwa madarakani kwa muda wote wa maisha yake.

Katika matokeo ya mwisho yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya taifa, kiasi cha asilimia 51 ya wapiga kura wamepinga mapendekezo hayo. Rais huyo wa Venezuela hata amesema ataendelea na ujenzi wa usishalist.

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld ameonya dhidi ya mtindo wa mageuzi wa Chavez na amesema hapo mapema kuwa kura hiyo ya maoni ingeweza kuleta kuporomoka kabisa kwa demokrasia nchini humo. Chavez ametishia kusitisha kuiuzia mafuta Marekani na kuitaifisha kampuni ya mafuta ya Hispania ya Repsol.