1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chavez awataka wananchi wake kuunga mkono mabadiliko ya katiba

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVPM

CARACAS.Rais Hugo Chavez wa Venezuela jana aliwataka wanaomuunga mkono kuyapigia kura mabadiliko ya katiba ambayo yatamuweka katika nafasi ya kuongoza maisha.

Kura juu ya mabadiliko hayo inatarajiwa kupigwa kesho ambapo Rais Chavez ametishia kuzuia usafirishaji wa mafuta nchini Marekani iwapo nchi hiyo itaingilia kati zoezi hilo la kesho.

Akiwahutubia zaidi ya wandamanaji laki mbili, Rais Chavez ambaye amekaa madarakani kwa miaka minane, alionya kuwa mahasimu wake wa ndani wanajaribu kuhujumu upigaji kura wa kesho kwa msaada kutoka Marekani.

Mjini Havana, Rais Fidel Castro wa Cuba ambaye ni swahiba mkubwa wa Chavez ameonya kuwa Marekani ina mipango ya kutaka kumuua Rais huyo wa Venezuela.

Castro katika tahariri yake kwenye gazeti la kikoministi la nchi hiyo amesema kuwa iwapo Marekani itatekeleza mpango huo, uchumi wa dunia utayumba.

Amesema kuwa alimuonya kiongozi huyo wa Venezuela juu ya njama za Marekani kutaka kumuua na kuchukua tahadhari ya kusafiri akiwa katika gari la wazi.