1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yalaani ziara ya ujumbe wa Marekani, Taiwan

Lilian Mtono
22 Februari 2024

Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya China kwenye Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Mike Garagher amesema bunge la taifa hilo linaiunga mkono kwa dhati Taiwan, baada ya mkutano na uongozi wa kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4cjjT
Taiwan Taipei | Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya China kwenye Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Mike Gallagher akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe Taiwan na Marekani wakati wa ziara
Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya China kwenye Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Mike Gallagher akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe Taiwan na Marekani wakati wa ziaraPicha: Ann Wang/REUTERS

Garagher, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa China ameongoza ujumbe wa wabunge watano waliokutana na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen na Makamu wa Rais Lai Ching-te.

Amesema anadhani Marekani ina jukumu la kukabiliana na kitisho kilichopo dhidi ya Taiwan huku akiionya China dhidi ya kukivamia kisiwa hicho akisema hatua hiyo itakuwa ni upuuzi wa hali ya juu.    

"Ni wazi kwamba kitisho kikubwa dhidi ya amani na utulivu katika mlango wa bahari wa Taiwan ni kuongezeka kwa uchokozi wa Chama cha Kikomunisti cha China. Hilo ndilo jukumu tulilonalo, la kuelewa kitisho hicho na kutafuta njia tunazoweza, kwa kuhusisha vyama vyote viwili nchini Marekani, kukikabiliana nacho ili kupata amani."

Soma pia:Taiwan yaripoti maputo manane katika anga zake
China kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Mao Ning, imelaani vikali ziara ya ujumbe wa Marekani katika kisiwa cha Taiwan ikiitaja kuwa ni "uingiliaji" na kuitaka  kuzingatia "sera ya China moja" kwa kuacha mazungumzo rasmi na Taiwan.