1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yasema kutambuliwa Palestina ni hatua muhimu

Tatu Karema
20 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, amesema leo kuwa juhudi za kukubaliwa kwa Palestina kama mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa ni hatua ya kurekebisha dhulma za muda mrefu dhidi ya watu wa Palestina

https://p.dw.com/p/4f0XI
Waziri wa mambo ya nje wa China Wany Yi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Beijing mnamo Aprili 1, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa China Wany YiPicha: PEDRO PARDO/AFP

Wang Yi ametoa kauli hiyo iliyoripotiwa na shirika la habari la China, Xinhua, wakati wa mkutano wa pamoja na mwenzake wa Papua New Guinea wakati wa ziara nchini humo.

Soma pia:Marekani yapiga kura ya turufu juu ya uanachama wa Palestina

Siku ya Alhamisi, Marekani iliuzuwia Umoja wa Mataifa kulitambua taifa la Palestina kwa kupiga kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja huo ya kuinyima mamlaka hiyo ya Palestina hadhi hiyo.