1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaunga mkono uchunguzi baada ya maandamano Hong Kong

Zainab Aziz | Sekione Kitojo
2 Julai 2019

Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu kwenye jengo la bunge la Hong Kong, wakitishia kuvuruga shughuli za serikali.

https://p.dw.com/p/3LRKg
HongKong Protest gegen Auslieferungsgesetz Polizei
Picha: picture-alliance/NurPhoto/V. Yuen

Waandamanaji Hong Kong wamevamia bunge la nchi hiyo katika maadhimisho ya leo ya mji huo kurejeshwa katika utawala wa China mwaka wa 1997, wakati kukiwa na hasira ya umma kuhusiana na sheria ambazo zitaruhusu watuhumiwa kupelekwa China bara kufunguliwa mashitaka.

Maandamano hayo yamekuwa ni  hatua ya moja kwa moja ya kuipinga serikali ya China kuwa na mkono wake katika uendeshwaji wa mji huo wenye mamlaka ya ndani. Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu kwenye jengo hilo, wakitishia kuvuruga shughuli za serikali lakini haikufahamika mara moja ni wangapi walibaki ndani.

Maelfu ya wanaharakati wa kidemokrasia walifanya maandamano mengine ya amani leo mchana, wakimkata kiongozi wa mji huo anayeegemea serikali ya China kujiuzulu na kubatilisha kile wanachokiona kuwa ni miaka mingi ya kushuka kiwango cha uhuru.

Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu kwenye jengo la bunge
Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu kwenye jengo la bungePicha: picture-alliance/AP Images/The Yomiuri Shimbun

Serikali Kuu ya China imelaani kitendo cha kulizingira bunge la Hong Kong na imesema inaunga mkono kufanyika uchunguzi wa jinai dhidi ya waandamanaji waliofanya ghasia.

Hong Kong ambayo ni kitovu cha shughuhuli za kifedha na yenye mamlaka ya ndani imekumbwa na  maandamano makubwa kwa wiki kadhaa sasa.

Waandamanaji hao wanapinga mswada wa sheria ya kuwezesha raia wa Hong Kong kupelekwa China endapo watatakiwa kujibu mashtaka mahakamani.

Hapo jana katika maadhimisho ya mwaka wa 22 tangu Uingereza kulirudisha jiji la Hong Kong katika mamlaka ya China, waandamani wenye misimamo mikali walivamia bunge na kuingia ndani kwa nguvu na  kutundika bendera ya enzi ya ukoloni wa Uingereza na kuchora huku wakiandna kuandika vitu vya kuipinga China.