1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Christian Wulff ateuliwa kugombea urais wa Ujerumani

Josephat Nyiro Charo4 Juni 2010

Ujerumani inaendelea na harakati za kumtafuta rais mpya wa nchi baada ya Hoerst Köhler kujiuzulu ghafla mwanzoni mwa wiki hii.

https://p.dw.com/p/NiQq
Christian Wulff, anayepigiwa upatu kuwa rais mpya wa UjerumaniPicha: AP

Viongozi walioko madarakani wanalazimika kumteua rais mpya kabla ya mwisho wa mwezi. Wakati huo huo, muungano wa vyama tawala vya CDU-CSU na Waliberali wa FDP wamemteua, Christian Wulff kugombea urais wa nchi. Christian Wulf aliye na umri wa miaka 50 ni kiongozi wa Jimbo la Lower Saxony, makao ya kiwanda cha kutengeneza magari cha Volkswagen.

Kwa upande wao vyama vya upinzani vinamuunga mkono Joachim Gauck, mwanaharakati wa kutetea haki za kiraia wa zamani na Mkurugenzi wa Shirika la kuhifadhi kumbukumbu za majasusi wa zamani wa Ujerumani, Stasi. Je hali hii inaashiria kipi? Nimezungumza na Abdallah Salim Mzee mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mkazi wa mji wa Potsdam ulio karibu na mji wa Berlin.