1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombia na Ecuador wamaliza mgogoro wa mpakani

8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DL08

SANTO DOMINGO:

Marais wa Colombia,Ecuador na Venezuela wamesema mgogoro wao uliohusika na kundi la waasi la FARC umemalizwa.Alvaro Uribe wa Colombia,Rafael Correa wa Ecuador na Hugo Chavez wa Venezuela walipeana mikono mbele ya waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wao wa kilele katika mji mkuu wa Jamhuri ya Dominika,Santo Domingo.

Juma lililopita,kiongozi mmojawapo wa ngazi ya juu wa FARC,Raul Reyes na waasi wengine 23 waliuawa na majeshi ya Colombia yaliyovuka mpaka wa Ecuador. Uvamizi huo ulizusha mgogoro wa kimataifa.FARC ni kundi kubwa kabisa la waasi nchini Colombia likiwa na kiasi ya wapiganaji 10,000 na linapigana vita vya chini kwa chini kwa zaidi ya miaka 40.