1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO : Jeshi lakanusha kutumia askari watoto

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCss
Mashambulio ya kigaidi mjini Madrid
Mashambulio ya kigaidi mjini MadridPicha: AP

Sri Lanka imekataa madai ya Umoja wa Mataifa kwamba sehemu ya wanajeshi wake imekuwa ikiwaandikisha askari watoto kupigana dhidi ya waasi wa Tamil Tiger.

Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa juu ya dhima ya watoto katika migogoro inayohusisha matumizi ya silaha amesema kamati yake imegunduwa ushahidi wa kuaminika kwamba wanajeshi wa usalama wamekuwa wakiwateka nyara watoto na kuwalazimisha kupigana.

Makao makuu ya jeshi ya Sri Lanka yamesema katika taarifa kwamba shutuma hizo hazina msingi na zinapotosha kabisa.

Umoja wa Mataifa unasema kwamba kundi liliomo ndani ya jeshi limewateka nyara watoto 135 tokea mwezi wa Mei katika jimbo la mashariki la Batticaloa.