1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Jeshi limezuia shambulio la waasi bandarini

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXX
Uwanja wa ndege wa Frankfurt
Uwanja wa ndege wa FrankfurtPicha: AP

Jeshi la wanamaji la Sri Lanka limefanikiwa kuzuia jeribio la waasi wa Tamil Tigers la kutaka kuishambulia bandari ya Colombo.Wizara ya ulinzi imesema,boti tatu zilijaribu kuingia katika eneo la ulinzi mkali katika bandari hiyo,licha ya wanamaji waliokuwa wakipiga doria kutoa amri ya kusimama.Ripoti zasema kuwa boti moja iliteketezwa na zingine mbili ziliweza kukimbia. Nchini Sri Lanka,mapigano makali yamezuka upya tangu mwaka jana licha ya kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini mwaka 2002. Zaidi ya watu 3,600 wamepoteza maisha yao katika mapigano hayo mapya.