1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Tamil Tigers wauwa wanajeshi 6

16 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FR

Wanajeshi 6 wameuawa na waasi wa Tamil Tigers nchini Sri Lanka katika eneo linalodhibitiwa na serikali,kusini mwa nchi.Maafisa wa kijeshi wamesema,mwanajeshi mwengine aliuawa alipokuwa akikusanya maiti za wenzake,baada ya kuripuka kwa bomu lililofukiwa ardhini.Wakati huo huo,ripoti za jeshi zinasema,waasi 30 wa Tamil Tigers waliuawa katika mapigano makali yaliyozuka siku ya Jumatatu,kaskazini mwa Sri Lanka.Katika kipindi cha miezi 23 iliyopita,zaidi ya watu 5,300 wameuawa katika mapigano yaliyotokea wilaya za kaskazini na mashariki kisiwani Sri Lanka.