1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Watu 29 wauawa katika mapigano mapya Sri Lanka

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPY

Watu wapatao 30 wameuawa kutokana na mapigano mapya katika peninsula ya Jaffna nchini Sri Lanka.

Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa wanajeshi wawili waliuawa kwa bomu lililotegwa njiani.

Wizara hiyo inatuhumu kuwa wapiganaji wa kitamil walitega bomu hilo.

Watu zaidi ya alfu 5 na mia nne wameshauawa nchini Sri Lanka kutokana na mipigano katika kipindi cha miezi 21 iliyopita.