1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cote d'Ivoire yaahidi uchaguzi huru na wa haki

Sekione Kitojo
30 Julai 2020

Tume ya uchaguzi Cote d'Ivoire imeahidi uchaguzi wa haki na salama wakati chama tawala kikimtaka rais Alassane Ouattara kugombea tena, akiwanyima watu wengine wanaotaka kuwania nafasi hiyo.

https://p.dw.com/p/3gAWA
Rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire
Picha: picture-alliance/dpa/S. Muylaert

Uchaguzi  unaonekana  kuwa  mtihani  mkubwa  wa udhabiti  uliopatikana  tangu  kulipotokea  vita  vya wenyewe kwa  wenyewe  nchini  humo  ambavyo vilisababisha  kuuwawa  kwa  watu 3,000  katika mwaka 2010  na  2011.

Mzozo kuhusiana  na  ushindi  wa  Ouattara  katika uchaguzi  wa  mwaka  2010 ulizusha  mzozo  na  vyama vya  upinzani  vinashuku  kwamba  ofisi  za tume ya uchaguzi ya nchi hiyo  inamuunga  mkono Ouattara.

Tume  ya  taifa  ya  Uchaguzi  inapanga  kufanya  mageuzi katika ofisi zake  na  kushauriana  na  vyama  vyote  katika wakati wa kuelekea  katika  uchaguzi, rais wa  tume  hiyo Ibrahime Coulibaly Kuibert, aliliambia  shirika  la  habari  la Reuters.