1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COVID-19 yarudi tena Ujerumani msimu wa baridi

Oliver Pieper | Iddi Ssessanga
18 Desemba 2023

Wajerumani wanasinasina na kukohoa kwa mara nyingine tena. Vipimo vya maji machafu vinaonyesha kuwa maambukizo ya COVID-19 yamefikia viwango vya juu zaidi tangu Juni 2022.

https://p.dw.com/p/4aJG1
Ujerumani| Kuanza kwa ufuatiliaji wa athari za Covi-19.
Magonjwa yanayoambukiza mifumo ya kupumua yameongezeka nchini UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa/M. Murat

COVID-19 imepoteza pakubwa sifa yake ya kutisha. Watu wengi nchini Ujerumani wamechanjwa au wamejijengea kinga ya msingi. Lakini pamoja na hayo, madaktari wa magonjwa ya jumla kama Lars Rettstadt wana shughuli nyingi.

"Ni msimu wa maambukizo tena. Kuna kusinasina na kukohoa sana," alisema daktari huyo mjini Dortmund, jiji la magharibi mwa Ujerumani. "Tunapofungua mlango Jumatatu asubuhi, kuna watu 70 wasio na miadi: wanaume, wanawake, vijana na wazee."

Kwa makadirio yake, asilimia 80 kati yao wana maambukizo ya virusi ya aina fulani. Nusu ya virusi hivyo ni COVID-19.

Bila amri ya kuvaa barakoa, wagonjwa wengi hawavai. Kliniki ya Rettstadt inawapatia kifaa hicho kwa euro senti 50. Ametenga saa moja tu kwa miadi ya mambukizo, na wagonjwa wanaweza pia kuwasiliana naye kwa video. Vipimo vya PCR vimehifadhiwa kwa wale walio katika hali mbaya haswa.

Soma pia: Ujerumani kulegeza vikwazo vya kuzuia maambukizi ya corona

"Hatuoni tena visa vikali," alisema, na kuongeza kuwa mgonjwa mmoja tu, mwenye umri wa miaka 94, alilazimika kulazwa hospitalini kwa sababu ya COVID-19.

Vinginevyo, dalili zinaonyesha aina ya baridi ya kawaida ambayo huwazuia watu kwenda kazini ili kupona kwa kujipumzisha kitandani nyumbani. Na licha ya hayo, bado siku za kuugua zinaweza kwenda kwa muda wa hadi wiki mbili.

Asilimia 10 ya nchi wanaugua magonjwa ya kupumua

Ingawa ugonjwa huu unaweza usiwe na kutisha, unasababisha usumbufu mkubwa. Kiasi cha asilimia 10 ya nchi ni wagonjwa, kulingana na taasisi ya afya ya umma ya Ujerumani, Robert Koch, na ofisi na taasisi za huduma zinapambana kusalia wazi.

Ongezeko la maambukizi ya COVID-19 Ujerumani

Na huku msimu wa Krismasi wa kuchanganyikana ukikaribia, Waziri wa Afya Karl Lauterbach amewataka watu kuimarisha chanjo zao.

Matukio rasmi, ya siku saba ni 38, ambayo yanaonekana kuwa ya chini ikilinganishwa na 2,000 wakati wa wimbi la omicron mapema 2022. Hata hivyo kwa kupima mara kwa mara, idadi hiyo inaweza kuwa haiwakilishi hali halis. Vipimo vya hivi karibuni vya maji machafu vimeonyesha COVID-19 zaidi majini tangu aina hii ya upimaji ilipoanza Juni 2022.

Aina nyingine za upimaji wa PCR zinaashiria matukio ya siku saba ya karibu 3,900 katika jimbo la magharibi la Ujerumani la Rhineland-Palatinate, alisema daktari wa virusi anayeishi Frankfurt Martin Stürmer. Idadi hii imepanda kutoka 2,600 wiki moja iliyopita.

"Tuko katika awamu ambapo takwimu za  virusi vya corona zinaongezeka sana," aliongeza.

Kirusi cha Pirola kinaongezeka

Takwimu za virusi vya corona ni mbali ya visa vya kawaida za mafua na magonjwa ya kupumua. Hata hivyo takwimu hizo hazijageuka kuwa mzigo mkubwa kwa hospitali na wadi za ICU, alisema Stürmer. Kiwango cha vifo pia kimeendelea kutobadilika.

Soma pia:Kesi ya udangayifu wa mamilioni kupitia vituo feki vya kupimia COVID 19 yaanza kusikilizwa Ujerumani 

Moja ya aina nyingi zilizopo sasa ni kirusi kidogo cha JN.1, kirusi kingine mrithi cha pirola, hivi sasa kinahusika kwa karibu theluthi moja ya visa vyote," aliongeza.

Ingawa hatari kwa watu kwa ujumla ni ndogo, Stürmer alitoa wito kwa makundi  yalioko hatarini, pamoja na watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60, kupata chanjo za ziada. Chanjo hizo zinaongeza safu ya ulinzi dhidi ya kile kinachoitwa COVID ya muda mrefu, ambacho ni athari za muda mrefu za COVID-19. Barakoa zinaweza kuleta mantiki, pia, aliongeza, ingawa kuna hamu ndogo ya umma ya kuzirejelea.

"Utayarifu wa kuchanjwa pia ni wa kiwango cha chini," alisema Stürmer. "Nadhani haya yote ni mambo ambayo tunaweza kuyaboresha kwa kiasi kikubwa kupitia mawasiliano chanya na yenye maana."

Chanzo: DW