1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CRAWFORD : Bush apiga hatua nzuri kwa mkakati wa Iraq

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfN
Wakimbizi nchini Kongo
Wakimbizi nchini KongoPicha: AP

Rais George W. Bush wa Marekani amesema amepiga hatua nzuri juu ya mkakati mpya kwa Iraq.

Kiongozi huyo wa Marekani alikuwa akizungumza kwenye shamba lake huko Crawford katika jimbo la Texas baada ya mazungumzo yake na washauri wake wa usalama wakiwemo Makamo wa Rais Dick Cheney,Waziri wa mambo ya nje Condoleezza Rice na Waziri mpya wa ulinzi Robert Gates.

Bush ameongeza kusema kwamba ana mashauriano mengi zaidi ya kufanya na kwamba utawala wake utazungumza na wabunge wa bunge la Marekani juu ya mkakati huo.

Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kutangaza mkakati wake mpya kwa Iraq hapo mwezi wa Januari.