1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR: Niger iache kushinikiza vyombo vya habari

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GG

Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari- IFJ-limetoa mwito kwa serikali ya Niger kusaidia kukomesha hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya vyombo vya habari nchini humo.Shirika hilo pia limemuomba Rais Mamadou Tandja,kuingilia kati na kumuachia huru mhariri Ibrahim Manzo na muandishi wa habari mwingine,Moussa Kaka.Mkurugenzi wa ofisi ya IFJ barani Afrika,Gabriel Baglo amesema, vyombo vya habari vinasumbuliwa tangu ulipoanza mgogoro wa kabila la Tuareg nchini Niger.