1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR:Wagombea urais nchini Senegal watiwa ndani

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXP

Askari polisi nchini Senegal wamepambana na waandamanaji katika mji mkuu Dakar.Vile vile wanachama 3 wa upinzani waliojiandikisha kugombea uchaguzi wa rais uliopangwa kufanywa Februari 25, wametiwa ndani.Maafisa wa polisi wamesema, wamelazimika kuchukua hatua kwani maandamano ya upinzani yamepigwa marufuku kwa sababu za usalama.Waandamanaji wanamtaka rais Abdoulaye Wade alie na umri wa miaka 80 aondoke madarakani. Wanamtuhumu kuwa anawafunga jela wapinzani wake wa kisiasa na mara kwa mara ameahirisha uchaguzi wa bunge uliotangazwa.