1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS : Rais Abbas akutana na Meshaal wa Hamas

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYy

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina na Kiongozi wa Hamas anayeishi uhamishoni nchini Syria Khaled Meshaal wamesema wamepiga hatua kubwa ya maendeleo katika mazungumzo yaliokuwa yakisubiriwa kwa muda mrfeu yaliofanyika mjini Damascus nchini Syria.

Mkutano huo umeshindwa kufikia makubaliano juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa lakini viongozi hao wamesema mazungumzo zaidi juu ya suala hilo yatafanyika katika kipindi kisichozidi wiki mbili.

Katika taarifa iliotolewa baada ya mazungumzo hayo wamesema wanapinga mapigano kati ya kundi la Hamas na Fatah la Rais Abbas.

Pande hizo mbili zimekuwa zikijaribu kwa miezi kadhaa sasa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika jitihada za kuifanya Marekani na Umoja wa Ulaya iondowe vikwazo vya misaada kwa serikali ya Palestina inayoongozwa na kundi la Hamas ambalo linagoma kuitambuwa Israel,kukanusha matumizi ya nguvu na kutii makubaliano ya amani yalioko hivi sasa kati ya Wapalestina na Israel.